Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema katika kujibu madai ya Marekani ya kwamba eti iko tayari kufanya mazungumzo na Iran na kuheshimu diplomasia na kusema: Huwezi kupiga nchi kwa mabomu na baadaye kudai eti unaheshimu mazungumzo ya kidiplomasia.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Tasnim, Ismail Baghaei, ameandika hayo kwenye ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa X kujibu madai ya Marekani dhidi ya Iran na kusema: Unapomnyooshea kidole kisicho cha haki mtu mwingine, kwa hakika vidole vingine vitatu vinakuelekea wewe.

Ameongeza kuwa: Tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Iran kamwe haziwezi kufunika jinai ya kushiriki moja kwa moja Marekani katika mauaji ya kimbari ya Wapalestina yanayoendelea hadi hivi sasa na kwenye vitendo ya kigaidi vinavyoendeshwa kitaasisi na hujuma za kuendelea za utawala wa Kizayuni dhidi ya nchi mbalimbali.

Baghaei amesema: “Kujivunia shambulio haramu dhidi ya vituo vya nyuklia vya matumizi ya amani vya Iran, kunaongeza tu dhima ya kimataifa inayobeba serikali ya Marekani kwa kufanya jinai hiyo na kunafichua hata chuki zaidi na uadui mkubwa wa watawala wa nchi hiyo dhidi ya taifa la Iran.”

Msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amefafanua zaidi kwa kuandika: “Madai ya Marekani kuhusu nia yake ya kuheshimu diplomasia na kufanya mazungumzo na sisi, si chochote ila ni udanganyifu na ulaghai wa wazi; mtu hawezi kupiga nchi kwa mabomu na halafu kujipa uthubutu wa kuzungumza kuhusu diplomasia na kudai anataka mazungumzo na kutatuliwa mambo kidiplomasia.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *