Baada ya Israel kushindwa kuzuia shambulio la droni la Yemen katika eneo la kusini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, gazeti la Jerusalem Post linalotoa nakala nyingi zaidi limekiri kuwa ulinzi wa anga wa Israel hauwezi kukabiliana na vipigo kutoka Yemen.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars; katika toleo lake la hivi karibuni kabisa lililotolewa baada ya shambulio jipya la ndege zisizo na rubani za Yemen katika maeneo mawili ya ardhi za Palestina zinayokaliwa kwa mabavu na kupelekea makumi ya Wazayuni kuwahishwa hospitalini, gazeti la Jerusalem Post limekiri kuwa jeshi la Yemen lina uwezo mkubwa wa kupenya mifumo ya ulinzi wa anga wa Israel na kufanya mashambulizi makali.

Gazeti hilo limeandika: “Wahouthi wanaendelea kugundua udhaifu wa Israel, na athari za mashambulizi yao zinaendelea kuonekana. Ni athari za uharibifu na hata kuua. Ndege zisizo na rubani za Yemen, ambazo ni za bei ya chini na hazina kasi kubwa kama makombora, zimesababisha uharibifu mkubwa kwa Israel.”

Ripoti ya gazeti maarufu zaidi la Israel, yaani Jerusalem Post pia imesema: “Vita vimekuwa vya muda mrefu sana na vitisho dhidi ya Israel vimeongezeka; Wahouthi wamefanikiwa kugundua mapungufu katika mifumo ya ulinzi wa anga ya Israeli.”

Pia gazeti hilo limekiri kwamba majeshi ya Yemen hayawezi kuzuiwa na kwamba suluhisho pekee na la kweli ni kumaliza vita na kwamba kila waziri wa vita wa israel anapotoa vitisho dhidi ya Yemen anazidi kujifedhehesha tu na kuonesha Israel haina uwezo wa kuzuia mashambulizi ya Yemen.

Ansarullah ya Yemen bado ni mtetezi imara wa wananchi wa Ghaza na imeendelea kusimama imara kukabiliana na jinai za kutisha za Israel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *