
Kuhukumiwa jela kwa miaka mitano rais wa zamani wa Ufaransa Nicholas Sarkozy, baada ya siku ya Alhamisi, kupatikana na kosa la kuwatumia wake wa karibu, kupata ufadhili wa kifedha kwa ajili ya kampeni zake za urais kinyume cha sheria mwaka 2007, kutoka kwa kiongozi wa zamani wa Libya Muammar Kaddafi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ahmad el-Gaddafi, binadamu yake kiongozi huyo wa zamani wa Libya, aliyekuwa afisa mkubwa jeshi wakati wa vita katika taifa hilo na kupelekea kuuawa kwake mwaka 2011, anataka nguvu kuelekezwa kuhusu mchango wa Sarkozy kufadhili na kuunga mkono matumizi ya jeshi kwenye vita hviyo.
Ahmad, anamtaka rais Emmanuel Macron kuanzisha uchunguzi, ili kubainika ni kwanini Ufaransa wakati huo ukiongozwa na Sarkozy, iliruhusu jeshi la nchi yake kuingilia vita vya Libya.
Aidha, anataka Sarkozy kufungwwa jela kwa kile anachosema alichangia pakubwa kuiharibu Libya, ambayo tangu kuuawa kwa Kdhafi haina utulivu wa kisiasa na kiusalama.
Katika hatua nyingine, baada ya hukumu dhidi ya Sarkozy mwenye umri wa miaka 70, sasa anasubiri tarehe 13 mwezi Oktoba, atakapofahamishwa ni gereza lipi atapelekwa kutumikia kufungo chake.
Rais huyo wa zamani, ametozwa pia faini ya Euro 100,000 na kupigwa marufuku kuhudumu serikalini.