Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa, ameonya kuwa nchi ya Sudan Kusini inaelekea kutumbukia katika machafuko mapya, wakati huu watu Zaidi ya elfu 2 wakiripotiwa kuuawa katika vurugu za mwanzoni mwa mwaka huu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa umerekodi mauaji ya watu zaidi ya elfu 1 na matukio 423 ya utekaji nyara yakiwemo zaidi ya 160 ya ubakaji kuanzia mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu, hili likiwa ni ongezeko la asilimia 59 kutoka mwaka jana, UN ikisema idade hii huenda ikawa kubwa zaidi.

Volker Turk amesema ofisi yake inahofia kuvunjika kwa mkataba wa amani wa mwaka 2018 kutokana na matukio ya hivi karibuni, ikiwemo mashtaka aliyofunguliwa makamu wa Kwanza w arais Riek Machar.

Aidha Turk alitoa wito kwa utawala wa Juba kuhakikisha unaendesha kwa haki kesi ya uahini inayomkabili Machar.

Kwenye tarifa yake, Turk amesema mapigano yaliongezeka tangu mwezi Machi, jeshi la Serikali likitekeleza mashambulio ya anga kwenye miji ya Upper Nile, Jonglei, Unit na Warrap, ambapo makazi ya watu, shume na hospital vimeharibiwa.

Turk amewaambia waandishi wa habari kuwa, kuongezeka kwa mashambulizi ya kiholela na vurugu za kikabila kwenye majimbo ya Warrap na Jonglei, kunazidisha wasiwasi wa kutokea vita nyingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *