A

Chanzo cha picha, Ritesh

Katika jiji la Ambikapur, jimbo la Chhattisgarh, India, watu wenye njaa hupata mlo kamili bila kulipa pesa bali kwa kubadilisha taka za plastiki walizozikusanya. Mgahawa huu maalum, unaoitwa Garbage Cafe au Mgahawa wa taka, ulizinduliwa mwaka 2019 ukibeba kauli mbiu “taka zaidi, ladha bora zaidi”.

Kila siku watu huleta mifuko ya plastiki, chupa na vifungashio vilivyotupwa. Kwa kilo moja ya taka za pplastiki hupata mlo kamili wenye wali, mboga mbili, chapati, saladi na achari. Nusu kilo ya plastiki hubadilishwa kwa kifungua kinywa kama sambusa au kitafunwa jamii ya maandazi.

Kwa kina mama kama Rashmi Mondal, Mgahawa huu umekuwa mwokozi. Awali aliwahi kuuza taka za plastiki kilo moja kwa rupia 10 pekee kiasi kisichotosha kabisa kumsadia kimaisha. Sasa anaweza kulisha familia yake moja kwa moja kupitia taka za plastiki anazokusanya mitaani.

Kutatua njaa na taka kwa pamoja

H

Chanzo cha picha, Ritesh

Maelezo ya picha, Wengi hupata chakula hapa kwa kulipa taka

Kwa mujibu wa Vinod Kumar Patel, msimamizi wa mgahawa huo kwa niaba ya Halmashauri ya Jiji la Ambikapur (AMC), lengo lilikuwa kutatua matatizo mawili: njaa kwa masikini na taka za plastiki mitaani. Wengi wanaonufaika ni wasio na makazi na wakusanyaji taka. Kwa wastani, watu zaidi ya 20 hulishwa kila siku.



Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *