Nchi ya Qatar, imetangaza kujitolea kwake kuhakikisha amani inarejea mashariki mwa DRC, na kanda nzima ya nchi za maziwa makuu.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Qatar, Mohammed bin Abdulaziz, amesema nchi yake imejitolea kuhakikisha amani inarejea mashariki mwa DRC, kupitia mazungumzo na mbinu nyingine, waziri Abdulaziz, akikariri kuwa nchi yake inaunga mkono vikamilifu mkataba wa Amani wa Washington.

Licha ya mazungumzo yanayoendelea ya kumaliza vita mashariki mwa DRC, mapigano yameendelea kuripotiwa nchini humo yakihusisha jeshi la serikali, vijana wa Wazalendo na waasi wa AFC M23.

Hili limechangiwa na misimamo mikali kutoka kwa serikali ya DRC na waasi wa M23, baadhi pia wakidai kuwa mazungumzo hayo yamekosa kuangazia chanzo cha mzozo ila yanalenga tu kutoa suluhu.

Mbali na masuala haya, jambo jingine linalotatiza upatikanaji wa usalama mashariki mwa DRC ni kutoaminiana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *