
Vuguvugu la maandamano nchini Madagascar limeenea katika miji kadhaa nchini kote siku ya Ijumaa Septemba 26, pamoja na Diego Suarez, ambapo makabiliano makali yaliripotiwa kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama. Mbali na mji mkuu, Antananarivo, miji kadhaa mikubwa ilikuwa chini ya amri ya kutotoka nje usiku wa jana.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Vuguvugu la waandamanaji wenye hasira lililoitikisa Madagascar, ambalo hapo awali lilijikita Antananarivo na Antsirabe, liliongezeka mnamo Septemba 26 katika miji mikuu ya pwani, anaripoti mmoja wa waandishi wetu huko Antananarivo, Guilhem Fabry. Huko Diego Suarez, kaskazini ya mbali, mamia ya wanafunzi wa chuo kikuu cha umma walikusanyika asubuhi. Jioni ya Septemba 26, vizuizi vya barabarani viliwekwa baada ya siku ya makabiliano makali, ambapo jengo la Wizara ya Fedha lilichomwa moto.
Matukio ya uporaji yaliripotiwa pia maeneo ya Tamatave na Majunga ambapo wanafunzi walikusanyika kwa wingi kudai haki yao ya maji na umeme. Waandamanaji walikuwa na mwelekeo wa familia zaidi huko Tulear, kusini. Miji yote hii imekuwa chini ya amri ya kutotoka nje tangu jioni ya Septemba 26.
Utulivu umerejea katika mji mkuu
Huko Antananarivo, vijana kutoka kwa kundi la Gen Z walitoa msaada kwa waathiriwa wa uporaji ili kusafisha uharibifu. Mji mkuu, ambao kwa kawaida ulikuwa na msongamano na kelele, haukuwa na watu kabisa mwisho wa siku amri ya kutotoka nje ilipokaribia. Shule ziliendelea zimefungwa siku nzima.
Hasira inaenea
Wakati uporaji ukiendelea siku nzima katika baadhi ya vitongoji vya mji mkuu, maandamano ya hasira pia yaliongezeka kote nchini. Katika mji wa Diego-Suarez ambapo makabiliano kati ya vikosi vya usalama na umma yalikuwa ya vurugu zaidi, kama Geoffrey, mkazi, anavyosimulia.
“Tulipoona kinachoendelea Tana, tulijua hali itakuwa ngumu, na sote tukaanza kuhifadhi vifaa. Ghafla, askari wa jeshi walifika. Niliona umati wa waandamanaji wakiweka vifusi barabarani ili kuweka vizuizi. Mapema saa 4 asubuhi, milio ya risasi ilisikika jijini. Wanafunzi walimbeba rafiki yao alifariki, ambaye aliuawa na polisi wa jiji. walikuwa wengi, nadhani, zaidi ya watu 2,000 walimleta kwenye makazi ya gavana wa mkoa wa Diana. Waliweka maiti mbele ya jengo hilo wakiwa na mabango yenye maandishi “Tunataka maji,” “Tunataka umeme,” na “Hatutaki ufisadi wowote.”
Rais wa Madagascar ahutubia taifa
Rais Andry Rajoelina alihutubia taifa jioni ya Septemba 26 na kutoa wito wa utulivu. Alisema yuko tayari kuwasikiliza vijana waliohamasishwa kutafuta suluhu la kukatika kwa umeme na uhaba wa maji. Alieleza kusikitishwa kwake na uchochezi wa kisiasa wa vuguvugu la amani la vijana. Kulingana na Rais Rajoelina, “mamluki walilipwa ili kupora na kuzua machafuko katika mji mkuu, kufuatia uchochezi wa wazi wa chuki na ghasia uliosambazwa siku chache mapema na viongozi wa upinzani kwenye mitandao ya kijamii.” Wakati wa hotuba hii ya dakika nane, alielezea ghasia za siku chache zilizopita kama vitendo vya uvunjifu wa amani, hata akimaanisha “aina ya mapinduzi ya kijeshi.” Pia alitangaza kumfukuza kazi Waziri wake wa Nishati na , Olivier Jean-Baptiste, ambaye alionekana kutowajibika.