
Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, raia zaidi ya 100 walitekwa nyara katika mkoa wa Ituri katika shambulio la wanamgambo wa Codeco jioni ya Jumatano, Septemba 24, 2025, huko Lidda, Wilaya ya Djugu. Wahasiriwa, wafanyabiashara, walikuwa wakirejea kutoka soko la Bule. Tukio hili la hivi punde linaongeza hali ya sintofahamu nchini.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Waathiriwa wengi walikuwa kwenye magari na pikipiki kabla ya kuvamiwa na wanamgambo wa Codeco.
Kiongozi wa shirika la kiraia la Bahema Nord, Charité Banza, anatoa wito wa kufanyika kwa operesheni ya pamoja ya FARDC na UPDF dhidi ya wanamgambo hao, ambao wanazusha ugaidi katika eneo hilo.
“Kulikuwa na watu zaidi ya 100 kwenye barabara hiyo. Jioni wafanyabiashara waliokuwa wakinunua bidhaa zao walikuwa kwenye malori na pia kulikuwa na pikipiki zilizokuwa na bidhaa, anasimulia. Wanamgambo kadhaa wa Codeco walifaya shambulio la kuvizia eneo la Lidda, wakawavamia wafanyabiashara hao, wakawavamia askari wa FARDCnyi waliokuwa wakisindikiza msafara huo.
Charité Banza anasikitishwa na utekaji nyara wa raia kadhaa na uporaji wa bidhaa. “Kwa vyovyote vile, hadi sasa tayari tumerekodi watu kadhaa ambaohawajulikani waliko. Zaidi ya 104, pikipiki iliyoporwa na wanamgambo hawa wa Codeco, pamoja na bidhaa ambazo wafanyabiashara hao walikuwa wamekwenda kununua huko Baule. Tumeona hali ngumu sana ambayo haiwezi kuvumilika.”