
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu siku ya Jumatatu tarehe 25 Agosti, alisema kuwa yuko tayari kupunguza “taratibu” uwepo wa jeshi la Israel nchini Lebanon ikiwa Beirut itatekeleza mpango wake wa kuwapokonya silaha Hezbollah.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Beirut, Paul Khalifeh
Matamshi ya Waziri Mkuu wa Israel yamekuja chini ya wiki moja kabla ya muda uliotolewa na serikali ya Lebanon kwa jeshi lake kuwasilisha mpango wa kukipokonya silaha chama cha Kishia. Hata hivyo, kiongozi wa chama kinachounga mkono Iran, Naim Qassem, amesisitiza tena kwamba kundi lake halitakabidhi silaha zake, licha ya uamuzi wa kulipokonya silaha ifikapo mwisho wa mwaka huu.
Badala ya kupokonywa silaha, Naim Qassem amedai kukomeshwa kwa uvamizi wa Israel, kukomeshwa kwa ukiukaji, kuachiliwa kwa wafungwa wa Lebanon nchini Israel, na kuanza kwa ujenzi wa vijiji vilivyoharibiwa wakati wa vita. Ni pale tu masharti haya yote yatakapotimizwa ndipo Hezbollah itakuwa tayari kujadili mkakati wa ulinzi wa taifa na mamlaka ya Lebanon.
Naim Qassem, hata hivyo, amepunguza ukali wa matamshi yake kwa kusema kwamba “jeshi la Lebanon ndilo linalowajibika kwa mstari wa mbele kwa ulinzi wa nchi,” na Hezbollah ikiwa “msaidizi.” Ili kutekeleza vyema kazi yake ya kulinda Lebanon, “jeshi lazima, hata hivyo, liwe na vifaa vya kutosha na kuungwa mkono.”
Ziara ya wajumbe wa Marekani
Kiongozi wa Hezbollah ameyasema haya katika mkesha wa ziara ya wajumbe wawili wa Marekani, Thomas Barrack na Morgan Ortagus, mjini Beirut, waliopewa jukumu la kufuatilia upokonyaji silaha wa chama hiki cha Kishia. Wajumbe wa Donald Trump watawapa viongozi wa Lebanon majibu ya Israel kwa ufafanuzi ulioombwa na Beirut.
Siku ya Jumatatu, Agosti 25, Benjamin Netanyahu alipendekeza uwezekano wa jeshi al Israel kujiondoa “hatua kwa hatua” katika ardhi ya Lebanon. Tangazo hili halionekani kutosheleza kuwashawishi Hezbollah kukabidhi silaha zake.