
Wanafamilia hao waliuawa baada ya makazi yao kulengwa katika mashambulizi hayo. Katika hatua nyingine, jeshi la Israel limeilipua nyumba ya mkaazi wa Kipalestina kwenye Ukingo wa Magharibi Muthanna Amro. Amro anatuhumiwa kufanya shambulizi lililowaua watu sita mjini Jerusalem.
Netanyahu asisitiza kuendelea kuishambulia Hamas Ukanda wa Gaza
Hayo yanajiri saa kadhaa baada ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuliambia baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuwa ni lazima nchi yake “ikamilishe kazi” dhidi ya wanamgambo wa Hamas ndani ya Gaza.
Israel inakabiliwa na shinikizo la kimataifa la kutaka kumaliza vita huko Gaza, huku mataifa mengine yakiendelea kutangaza kuitambua palestina kama taifa huru hatua inayopingwa vikali na Netanyahu.