
Kupitia gazeti la Rheinische Post lililochapishwa Jumamosi Dobrindt ameeleza kuwa wanaotakiwa kurejeshwa Syria ni pamoja na wahalifu wakifuatiwa na watu wasio na vibali halali vya kuishi Ujerumani. Waziri huyo ameongeza kuwa mazungumzo yanatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Michakato ya maombi ya hifadhi ya Wasyria iliyositishwa kuanza tena
Amebainisha kuwa, ameshaielekeza ofisi ya uhamiaji na wakimbizi kuanza tena michakato iliyositishwa ya waomba hifadhi wa Syria ili kuruhusu utaratibu wa kuwarejesha wanaostahili kuanza. Ujerumani haijawahi kumrejesha raia yeyote wa Syria nyumbani tangu mwaka 2012.