Hata hivyo Wizara ya Ulinzi ya Denmark haijabainisha mahali hasa zilikoonekana droni za hivi karibuni.Vyombo kadhaa vya habari nchini humo vyenyewe vimearifu kukuonekana kwa droni karibu na kambi ya Karup ya jeshi la anga.

Ujerumani nayo imesema droni kadhaa zimeonekana katika jimbo la Schleswig-Holstein linalopakana na Denmark Alhamisi kuamkia Ijumaa. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Alexander Dobrindt amesema kitisho cha droni ni kikubwa na kuwa Ujerumani itachukua hatua za kujilinda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *