Waziri Mkuu wa Israel anatarajia kukutana leo Jumatatu na mwenzake wa Marekani Donald Trump kuhusu vitra vya Gaza, baada ya kuelemewa na ukosoaji kutoka nje ya nchi kutokana na vita hivyo. Hata hivyo Benjamin Netanyahu anakabiliwa na shinikizo kutoka ndani ya nchi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu atatetea nia yake ya “kumaliza kazi” huko Gaza atakapokutana na Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumatatu.

Mkutano huo unakuja siku chache baada ya Trump kufichua mpango wenye vipengele 21 unaolenga kumaliza vita katika ardhi ya Palestina wakati wa majadiliano na viongozi wa Kiarabu na Kiislamu kando ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Siku ya Jumapili, Trump alidokeza “kitu maalum” kuja katika mazungumzo ya Mashariki ya Kati, akiongeza katika chapisho kwenye jukwaa lake la Truth Social: “TUTAFANYA HIVYO!!!”

Siku ya Ijumaa, Trump aliwaambia waandishi wa habari mjini Washington “Nadhani tuna mpango” kuhusu Gaza, kama vile Netanyahu, akizungumza katika Umoja wa Mataifa, aliapa “kumaliza kazi” katika vita vya Israel dhidi ya Hamas.

Lakini wataalam wameliambia shirika la habari la AFP kwamba Netanyahu alionekana kuzuiwa, akikabiliwa na ongezeko la wito wa kimataifa na wa ndani wa kumaliza vita.

“Hana chaguo lingine ila kukubali” mpango wa Trump wa kusitisha mapigano, amesema Eytan Gilboa, mtaalamu wa mahusiano ya Marekani na Israel katika Chuo Kikuu cha Israel cha Bar-Ilan.

“Kwa sababu tu Marekai na Trump wamesalia karibu mshirika wake wa pekee katika jumuiya ya kimataifa.”

– “Makubaliano ya kina” –

Nchini Israel, makumi ya maelfu ya waandamanaji wamemshinikiza Netanyahu akubali kusitisha mapigano, na Jumamosi walimtaka Trump kutumia ushawishi wake.

“Kitu pekee ambacho kinaweza kusimamisha mtelezo ndani ya shimo ni makubaliano kamili na ya kina ambayo yanamaliza vita na kuwaleta mateka wote na wanajeshi nyumbani,” amesema Lishay Miran-Lavi, mke wa Omri Miran, ambaye bado yuko mateka huko Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *