Takriban watu wanne wameuawa siku ya Jumapili, Septemba 28, na mtu aliyefyatua risasi wakati wa ibada katika kanisa la Mormon huko Michigan, kaskazini mwa Marekani, kulingana na idadi mpya ya vifo iliyotangazwa na polisi. Idadi ya vifo vya awali ya watu wawili ilikuwa imetangazwa, kanisa lilipochomwa moto na mshukiwa ambaye mwenyewe aliuawa kwa kupigwa risasi.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Miili mingine miwili ” ilipatikana kwenye vifusi vya kanisa lililochomwa moto na mshukiwa, mkuu wa polisi wa jiji la Grand Blanc amesema katika mkutano na waandishi wa habari. “Hii inafanya jumla ya waathiriwa kufikia wanne,” ameongeza. Mshukiwa, Thomas Jacob Sanford, 40, aliuawa kwa kupigwa risasi na vikosi vya usalama dakika nane baada ya shambulio hilo kuanza. Kanisa hilo lililoko katika Kitongoji cha Grand Blanc, Michigan, kaskazini mwa Marekani, pia lilichomwa moto, polisi wamesema, bila kutoa sababu ya mauaji hayo.

“Hili linaonekana kuwa shambulio lingine lililolengwa dhidi ya Wakristo nchini Marekani,” rais wa Marekani amesema kwenye mtandao wake wa Truth Social. “Janga hili la ghasia katika nchi yetu lazima likomeshwe mara moja,” ameongeza, chini ya wiki tatu baada ya mauaji ya mshawishi wa kihafidhina Charlie Kirk.

Kulingana na Mkuu wa Polisi wa Grand Blanc William Renye, watu wanane pia walijeruhiwa na kulazwa hospitalini. Saba walikuwa katika hali nzuri na mmoja katika hali mbaya kufikia alasiri. “Tunatarajia kupata waathiriwa zaidi mara tutakapolinda eneo la tukio,” mwakilishi wa vikosi vya usalama alisema saa sita mchana.

FBI iliwasili mara moja katika eneo la tukio na itaongoza uchunguzi wa shirikisho, huku ikitoa msaada wake kamili kwa mamlaka za eneo hilo na kikanda,” Donald Trump amesema.

Kuibuka tena kwa vurugu za kisiasa nchini

“Wacha tuwaombee wahasiriwa,” Makamu wa Rais JD Vance amesema kwenye mtndao wa kijamii wa X. “Vurugu kama hii katika sehemu ya ibada ni ya kushangaza na ya kutisha.” “Nawaalika mjiunge nami kuwaombea wahasiriwa wa janga hili baya,” amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali Pam Bondi kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Marekani imekumbwa na ongezeko kubwa la ghasia za kisiasa katika miaka ya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na mauaji ya Charlie Kirk mnamo Septemba 10, ambayo yalizidisha mvutano. Bila kujua mara moja nia gani, kambi ya mrengo wa kulia ya Donald Trump ilimshutumu haraka kambi ya mrengo wa kushoto kwa kuusika kwa hali ya vurugu na ikataja “ugaidi wa nyumbani” wa mrengo wa kushoto.

Shambulio hilo dhidi ya kanisa la Mormon linakuja mwezi mmoja baada ya shambulio la mwishoni mwa Agosti kwenye kanisa lililo karibu na shule ya Kikatoliki huko Minneapolis, Minnesota (kaskazini). Watoto wawili waliuawa na karibu watu ishirini walijeruhiwa. Pial inakuja wakati Rais Trump anaongeza juhudi za kupeleka kikosi cha walinzi wa taifa huko Chicago, mji mkuu wa Michigan, na miji mingine kote Marekani, ambayo mara nyingi inatawaliwa na kambi ya upinzani ya Democratic.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *