
Matokeo ya uchaguzi wa wabunge wa Septemba 27, 2025, yametangazwa usiku wa Septemba 28. Chama cha Democratic Union of Builders (UDB), chama cha Rais Oligui Nguema, ndicho kinaongoza. Kimeshinda wapinzani wote wakuu lakini kililazimishwa katika raundi ya pili katika viti kadhaa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Libreville, Yves-Laurent Goma
Siku ya Jumapili jioni, Waziri wa Mambo ya Ndani amesoma matokeo yaliyo wazi ya uchaguzi wa wabunge, jimbo kwa jimbo, lakini bila kutoa takwimu za jumla. Amebainisha kuwa kati ya viti 145 vinavyogombaniwa, matokeo ya zaidi ya viti ishirini bado yanasubiri, na kwamba chaguzi tatu zitapaswa kurudiwa.
Baadhi ya matokeo yanaonyesha mafanikio ya Chama cha Democratic Union of Builders (UDB), chama cha Rais Oligui Nguema. Chama kilichoanzishwa miezi mitatu tu iliyopita na rais wa sasa wa Gabon, Brice Clotaire Oligui Nguema, kimepata idadi kubwa ya wawakilishi waliochaguliwa katika duru ya kwanza. Inafuatwa na PDG, chama kilichoondolewa mamlakani katika mapinduzi ya Agosti 30, 2023.
PDG, ambayo ilitawala Gabon kwa zaidi ya nusu karne, ina idadi kubwa zaidi ya wagombea waliofuzu katika duru ya pili. Watamenyana na UDB mnamo Oktoba 11.
Chama cha Paulette Missambo, rais wa Baraza la Seneti la mpito, na chma cha Alexandre Barro Chambrier, makamu wa rais wa serikali ya Gabon na kiongozi wa tatu wa nchi hiyo, vitawakilishwa vyema katika Bunge la taifa. Vyama kadhaa vya zamani havikupata chochtee.
Mzozo wa uchaguzi unaonekana kuwa athari.
Hata hivyo matokeo lazima yathibitishwe au kukataliwa na Mahakama ya Kikatiba. Mzozo wa uchaguzi huenda ukawa mkubwa, huku shutuma za udanganyifu zikiongezeka kote nchini.
Raia wa Gabon waliitwa kupiga kura siku ya Jumamosi katika chaguzi za mitaa na wabunge, chaguzi mbili ambazo zinakamilisha mpito wa kisiasa ulioanza baada ya mapinduzi ya Agosti 2023 ambayo yalimaliza miaka 55 ya ukoo wa Bongo madarakani.