
Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambulizi wa Bournemouth Antoine Semenyo anaendelea kuvutia nia licha ya kusaini kandarasi mpya msimu wa joto, huku Tottenham, Manchester United, Manchester City na Aston Villa zikimhitaji mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (TBRFootball)
Arsenal wako kwenye mazungumzo na winga Bukayo Saka, 24, kuhusu kandarasi mpya ambayo itamfanya kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa pesa nyingi zaidi klabuni hapo. (Express External,)
Newcastle wanataka kumpa beki wa zamani wa Uingereza Kieran Trippier mkataba mpya. Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 unamalizika mwishoni mwa msimu huu. (Chronicle, external)

Chanzo cha picha, Getty Images
Barcelona itasubiri kufanya uamuzi kuhusu kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, 27, kwa msingi wa kudumu. (Football Insider,)
Nia ya Liverpool ya kutaka kumsajili Dayot Upamecano wa Bayern Munich, 26, mwezi Januari inaweza kuyumba huku klabu hiyo ya Bundesliga ikiwa na nia ya kumsainisha beki huyo wa kati wa Ufaransa kwa mkataba mpya. (Football Insider,)
Tottenham, Chelsea na Brighton wanavutiwa na mshambuliaji wa Brazil Rayan, 19, anayechezea Vasco da Gama. (Football Insider)

Chanzo cha picha, Getty Images
Spurs pia wana nia ya kumnunua Arda Guler wa Real Madrid. Kiungo huyo wa kati wa Uturuki mwenye umri wa miaka 20 ametatizika kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha Real na anatakiwa pia na Newcastle na Arsenal. (Fichajes – In Spanish)
Vilabu vinavyoshiriki michuano ya Preston, Derby na Hull vina nia ya kumsajili winga wa Brighton Muingereza Tom Watson, 19, kwa mkopo mwezi Januari. (Lancashire Post)
Imetafsiriwa na Seif Abdalla