#HABARI: Wajumbe wa Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika wa Korosho (KCJE LTD), wameendelea na ziara yao ya kutembelea vyama vingine vya ushirika wa mazao nchini, kwa lengo la kujifunza mbinu bora za uendeshaji na kudumisha ushirika.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa KCJE LTD Bw. Mabruck Mpangule, amesema kuwa ziara hiyo imelenga kuimarisha uelewa wa wajumbe kuhusu namna vyama vingine vya ushirika nje ya tasnia ya Korosho vinavyofanikisha shughuli zao na kuwahudumia wanachama.

KCJE LTD imepata mafanikio makubwa katika kipindi kifupi tangu kuanzishwa, ikiwemo kuagiza pembejeo za ruzuku kwa wakulima wa korosho kwa miaka mitatu mfululizo, hatua hiyo imechochea ongezeko la uzalishaji wa korosho pamoja na kuinua bei ya zao hilo kwa wakulima, KCJE LTD ni ushirika unaojumuisha vyama vikuu vya korosho nchini, na unaendelea kuonesha dhamira ya dhati ya kuendeleza kilimo cha korosho kwa njia shirikishi na endelevu.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *