Waandamanaji kutoka Israel wametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano kwenye ukanda wa Gaza na kuachiwa kwa mateka.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wanahabari kutoka shirika la Habari la AFP, wameshuhudia waandamanaji wakifunga barabara jijini Tel Aviv, wakiwa na mabango kupaza sauti zao, huku wengine wakionekana kwenye Ubalozi wa Marekani.

Maandamano haya yanakuja baada ya serikali ya Israel, kutangaza mpango wa kudhibiti mji wa Gaza ambapo wakaazi, wamehama.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu anasema atakubali mpango wa kusitisha vita kwa siku 60 kama ilivyopendekezwa na wasuluhishi na kukubaliwa na Hamas iwapo, mateka wote wataachiwa huru.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *