Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban anajulikana kwa ukaribu wake na Moscow: anakataa kutoa msaada wa kijeshi kwa Kyiv na mara kwa mara anazuia mazungumzo ya kujiunga na Ukraine na Umoja wa Ulaya. Mvutano kati ya nchi hizo mbili unaongezeka kutokana na kupaa kwa ndege zisizo na rubani za Hungary katika eneo la Ukraine.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kutoka kwa mwandishi wetu huko Budapest, Florence La Bruyère

Kwa mujibu wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ndege isiyo na rubani ya Hungary iliingia katika anga ya Ukraine siku tatu zilizopita. Nchi hizo mbili ni majirani: Hungary inashiriki mpaka wa kilomita 140 na Ukraine. Kwa mujibu wa Rais Zelensky, ndege hiyo isiyo na rubani ya Hungary iliruka juu ya mitambo ya viwanda katika eneo la Ukraine la Zakarpattia.

Mgogoro wa kidiplomasia kati ya Kyiv na Budapest

Kutokana na shutuma hizi za Ukraine, Waziri wa Mambo ya Nje wa Hungary amekanusha madai hayo. Lakini mwenzake wa Ukraine amejibu kwa kuonyesha ramani inayoonyesha wazi ndege isiyo na rubani ya Hungary katika anga ya Ukraine. Naye Andri Sybiha, waziri wa mambo ya nje wa Ukraine, amesisitiza: “Vikosi vyetu vya kijeshi vimekusanya ushahidi wote muhimu, na bado tunasubiri Hungary kuelezea nini kitu hicho kilifanya katika anga yetu.”

Siku ya Jumatatu, Septemba 29, katika podikasti iliyowalenga wapiga kura wake, Viktor Orban alisema, “Hebu tukubali kwa mfano kuwa ndege zisizo na rubani za Hungary zilivuka mpaka. sasa mnataka nini?” Kwa hiyo Orban hakukanusha tukio hilo, bali alilidharau. Aliongeza: “Ukraine si nchi huru na inayojitawala; sisi ndio tunaiweka sawa, kwa hivyo haipaswi kujiendesha kana kwamba inajitegemea.” Hii si mara ya kwanza kwa Waziri Mkuu wa Hungary kutilia shaka uhuru wa Ukraine. Orban hapo awali alibainisha kwamba Ukraine ni kama eneo la Urusi, kana kwamba alitaka kumuunga mkoo Vladimir Putin na kuonysha kuwa yuko sahihi.

Maafisa wa idara ya ujasusi wanaohusishwa na wachache wa Hungary nchini Ukraine

Haijulikani ikiwa hii ilikuwa hitilafu ya mpango kwenye ndege isiyo na rubani au ilikusudiwa. Lakini mwezi wa Mei mwaka jana, mamlaka ya Ukraine iliwakamata majasusi wawili katika eneo lao, raia wawili wa Ukraine wa kabila la wachache kutoka Hungary. Kulingana na Kyiv, walikuwa wameajiriwa na idara ya ujasusi ya Hungary kukusanya habari kuhusu kambi za kijeshi na mifumo ya ulinzi wa anga kusini magharibi mwa Ukraine, karibu na mpaka wa Hungary.

Mnamo Agosti 21, kwa mara ya kwanza, Urusi ilishambulia kiwanda cha vifaa vya elektroniki katika eneo hili la kusini-magharibi mwa Ukraine. Upinzani wa Hungary na wachambuzi huru walihoji mara moja ikiwa serikali ya Viktor Orban ilikuwa ikiipeleleza Ukraine kutoa ujasusi wa kijeshi kwa Urusi. Hili ni swali kubwa, ambalo, kwa sasa, hakuna mtu anayeweza kujibu kwa uhakika.za viwandani, nguo, magari ya Afrika Kusini, mazao ya kilimo, na hata rasilimali za madini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *