
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amekanusha kukubali kanuni ya taifa la Palestina katika video iliyorushwa leo Jumanne, Septemba 30, kwenye akaunti yake ya Telegram baada ya kuwasilishwa kwa mpango wa amani wa Rais Donald Trump wa Gaza.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Sijakubali hata kidogo, na haikuandikwa katika makubaliano,” Benjamin Netanyahu amesema akijibu swali kuhusu iwapo “amekubali taifa la Palestina,” “lakini jambo moja liliwekwa wazi [wakati wa mazungumzo na Donald Trump]: tutapinga vikali taifa la Palestina.”
Mpango wa Gaza uliowasilishwa na Donald Trump unaeleza kwamba “masharti yanaweza kufikiwa ili kufungua njia ya kuaminika kuelekea kujitawala na kuanzishwa kwa taifa la Palestina.”
Hata hivyo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema anaunga mkono pendekezo la mpango wa amani kwenye Ukanda wa Gaza baada ya mazungumzo na Rais Trump siku ya Jumatatu
Ikulu ya White House jana Jumatatu ilitangaza mpango wa amani wenye pointi 20 ambazo ni pamoja na kuwanyang’anya kabisa silaha Hamas, Israel kujindoa taratibu kwenye Ukanda wa Gaza.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari Trump aidha alisema ataanzisha baraza la amani atakaloliongoza, litakalosimamia kipindi cha mpito kwenye Ukanda wa Gaza.
Hamas imeanza kutathmini mpango wa amani wa Donald Trump kwa Gaza leo Jumanne. Chanzo kutoka Palestina kilicho karibu na Hamas kimesema Jumanne kwamba vuguvugu la Kiislamu limeanza “msururu wa mashauriano” juu ya mpango huo, ambao unaweza “kudumu kwa siku kadhaa.”