Miaka sita baada ya kufunguliwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ramon kwa kelele na mbwembwe nyingi, ukiwa ni uwanja wa ndege wa pili kwa ukubwa wa utawala wa Kizayuni, sasa hivi mashambulizi ya wanamapambano ya Yemen yamepelekea kufungwa kabisa uwanja huo kama sehemu ya Operesheni Kimbunga cha Al-Aqsa iliyoongozwa na HAMAS miaka miwili iliyopita.

Uwanja wa Ndege wa Ramon, ambao ulitakiwa kuwa lango la kimataifa la kuufikia moja kwa moja mji wa Eilat kwenye pwani ya Bahari Nyekundu, siku hizi umetelekezwa kikamilifu, hakuna ndege za kimataifa zinazotumia uwanja huo, zilizobakia ni safari chache tu za ndani zinazofanyika kila wiki.

Wazayuni walitumai kwamba kwa kufungua uwanja huo wa ndege uliogharimu mabiliioni ya dola, wangeiunganisha Israel na miji mikuu ya Ulaya na kuvutia makumi ya maelfu ya watalii wa kigeni kila mwaka, lakini ndoto hiyo ilififia haraka tangu HAMAS ilipoongoza operesheni ya kihistoria ya Kimbunga cha al Aqsa mwezi Oktoba 2023. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ramon, ambao uko umbali wa kilomita 18 tu kutoka bandari ya Eilat, ulifunguliwa mwaka 2019 kwa lengo la kupaisha uchumi wa Israel, lakini matokeo yamekuwa kinyume chake.

Uwanja huo wa ndege ulikuwa na maduka makubwa na mikahawa na ulikuwa na uwezo wa kupokea makumi ya ndege kutoka sehemu tofauti za ulimwengu kwa wakati mmoja. Hata hivyo, ushahidi unaonesha kwamba nguvu za makombora na ndege zisizo na rubani wa jeshi la Yemen ambalo linatoa vipigo vya mtawalia kwenye mji wa Eilat na mengineyo ya ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel, zimepelekea kupata hasara kubwa Israel. Takriban hakuna ndege za moja kwa moja za kimataifa zinazopaa au kuwasili kutoka uwanja huo wa ndege. Uwanja huo sasa unatumika tu kuhamisha walowezi wa Kizayuni na kuwapeleka Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion mjini Tel Aviv.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *