
Vyama vya wafanyakazi nchini Madagascar vinaongeza shinikizo kwa Rais Andry Rajoelina, wiki moja baada ya kuanza kwa vuguvugu la maandamano ambalo halijawahi kushuhudiwa linaloitikisa taifa hivi sasa. Mshikamano wa Vyama vya Wafanyakazi vya Madagascar, jukwaa kuu la vyama vya wafanyakazi nchini, umeitisha mgomo mkuu siku ya Jumatano, tarehe 1 Oktoba. Kama vile kundi la vuguvugu la vijana wa Gen Z, pia linatoa wito wa kujiuzulu kwa mkuu wa nchi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu wa Antananarivo, Guilhem Fabry
Walimu, wahudumu wa afya, maafisa wa forodha… Mshikamano wa Vyama vya Wafanyakazi vya Madagascar unaleta pamoja vyama vya wafanyakazi zaidi ya hamsini, vinavyowakilisha wafanyakazi wa serikali. Kwa mara ya kwanza, siku ya Jumatano, Oktoba 1, jukwaa hili liliitisha maandamano katika mitaa ya Antananarivo. Kulingana na mkuu wa jukwa hilo, Herizo Andrianavalona Ramanambola, wafanyakazi zaidi ya elfu waliitikia wito wake.
Miongoni mwa madai yao: ongezeko la mishahara ya watumishi wa umma, iliyozuiwa tangu mwaka 2022 nchini Madagascar, pamoja na kuheshimiwa kwa uhuru wa vyama vya wafanyakazi na uhuru wa kujieleza. Jukwaa hilo, ambalo linajihusisha na uhamasishaji wa kundi la Gen Z, linataka kuwahimiza watumishi wa umma kuandamana kila siku hadi Rais Andry Rajoelina atakapojiuzulu. Linatumai kuchangia katika kutatua mgogoro huo kupitia mashauriano mapana.
Wakati wakiunga mkono maandamano yanayoongozwa na vuguvugu la vijana wa Gen Z, majukwaa mengine ya vyama vya wafanyakazi-kama vile FISEMA-hata hivyo yanasitasita kuitisha mgomo mkuu, wakihofia kwamba utazidisha hatari ambayo tayari inawakabili wafanyakazi.