Marekani itapanga kuipatia Ukraine taarifa za kijasusi zitakazotumika kuratibu mashambulizi ya makombora ya masafa marefu dhidi ya miundombinu ya nishati ya Urusi, maafisa wawili wamesema siku ya Jumatano, wakati nchi hiyo ikifikiria kuitumia Kyiv makombora ambayo yanaweza kutumika katika mashambulio hayo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa gazeti la The Wall Street Journal, maafisa wa serikali ya Marekani wamenukuliwa wakieleza kuwa hatua hiyo inazingatiwa wakati Washington ikitathmini uwezekano wa kuipatia Kyiv silaha zaidi zenye uwezo wa kushambulia kwa umbali mrefu.

Marekani pia inawaomba washirika wake wa NATO usaidizi kama huo, maafisa hao wamesema.

Hatua hiyo ni mabadiliko ya kwanza ya sera inayojulikana kuidhinishwa na Rais Donald Trump tangu kuongeza shinikizo kwa Urusi katika wiki za hivi karibuni, kwa lengo la kumaliza vita vya zaidi ya miaka mitatu vya Moscow katika nchi jirani ya Ukraine.

Washington kwa muda mrefu imekuwa ikishiriki taarifa za kijasusi na Kyiv, lakini sasa itakuwa rahisi kwa Ukraine kushambulia miundombinu kama vile viwanda vya kusafishia mafuta, mabomba na mitambo ya kuzalisha umeme ili kuinyima Kremlin mapato na mafuta.

Trump ameshinikiza nchi za Ulaya ziache kununua mafuta ya Urusi badala ya makubaliano yake ya kuiwekea vikwazo vikali Moscow katika jaribio la kukata ufadhili wa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Ikulu ya Marekani wala uwakilishi wa Ukraine kwa Umoja wa Mataifa hawajibu mara moja maombi tofauti ya maoni. Ujumbe wa Urusi kwa Umoja wa Mataifa huko New York ulikataa kutoa maoni.

Uamuzi huu unakuja wakati Marekani pia inazingatia ombi la Ukraine kwa kuipa makombora ya Tomahawks, ambayo yanakwenda umbali wa kilomita 2,500, zinazotosha kufika Moscow na sehemu kubwa ya Urusi ya Ulaya ikiwa itarushwa kutoka Ukraine.

Ukraine pia imeunda kombora lake la masafa marefu, Flamingo, lakini idadi ya makombora hayo haijulikani, kwani kombora hilo liko katika awamu ya uzalishaji.

Kwa mujibu wa maafisa wa Marekani, kuidhinishwa kwa taarifa za ziada za kijasusi kumekuja muda mfupi kabla ya Trump kuchapisha taarifa kwenye mtandao wa kijamii wiki iliyopita akipendekeza Ukraine inaweza kuchukua tena maeneo yake yote kutoka kwa Urusi, na hivyo kuashiria mabadiliko makubwa ya matamshi makali kwa mafufaa ya Kyiv.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *