
Shirika la Afya Duniani( WHO) limetangaza kuwa mlipuko wa wa ugonjwa wa Ebola kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo unaonyesha “dalili za kupungua kwa maambukizi”.
Katika ripoti yake kuhusu hali ya mambo, Ofisi ya Kikanda ya WHO barani AFrika imeeleza kuwa katika wiki mbili zilizopita, kesi chache za Ebola ziliripotiwa miongoni mwa watoto.
Ripoti hiyo imebainisha kuwa kuanzia tarehe 28 mwezi Septemba mwaka huu, jumla ya kesi za Ebola 64 zikiwemo 53 zilizothibitishwa na 11 zilizokuwa zikishukiwa zimesajiliwa katika Ukanda wa Afya wa Bulape katika jimbo la Kasai.
Wakati huo huo watu 42 wamethibitishwa kuaga dunia kwa ugonjwa huo. Maafisa wa afya nchini Kongo tarehe 4 Septemba walitangaza mlipuko wa 16 wa Ebola katika jimbo la Kasai linalopakana na Angola.
Watu tisa waliokuwa wanaugua Ebola wameruhusiwa kurudi nyuma baada ya kupatiwa matibabu hospitalini na wengine 13 wanaendelea kupatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa WHO,kesi tano zilizothibitishwa zimeripotiwa kati ya wahudumu wa afya, ikiwa ni pamoja na vifo vitatu.
Tangu kuanza kwa mlipuko, wanawake wanatakwa kuambukizwa pakubwa Ebola idadi ambayo ni sawa na 57.8%, huku watoto wenye umri wa kuanzia sifuri hadi miaka tisa wakiunda asilimia 25.
Mlipuko wa ugonjwa wa Ebola bado upo katika maeneo sita ya afya kati ya 21 yanayounda Ukanda wa Afya wa Bulape.