
Maandamano makubwa yameshuhudiwa katika nchi za Ulaya kupinga mashambulizi ya utawala wa Israel dhidi ya uvamizi wa meli ya msafara wa kimataifa wa Sumud.
Maandamano hayo yamelaani vikali kitendo cha utawala ghasibu wa Israel cha kuivamia kijeshi msafara wa kimataifa wa meli unaojulikana kama Sumud uliokuwa ukielekea Ukanda wa Gaza kwa ajili ya kufikisha misaada ya kibinadamu na kuvunja mzingiro Tel Aviv dhidi ya Ukanda wa Gaza.
Kwa mujibu wa ripoti, maandamano haya yamefanyika nchini Italia, Ubelgiji, Ujerumani, Ufaransa, Ugiriki, Uturuki na nchi nyingine za Ulaya.
Boti nyingi za msafara wa kimaataifa wa meli zipatazo 50 unaojulikana kama (Sumud) zilivamiwa jana na jeshi la wanamaji la Israel zilipokuwa zikikaribia katika ukanda wa pwani.
Idadi isiyojulikana ya wanaharakati wa msafara huo wa kimataifa walitiwa mbaroni na mawasiliano ya meli hizo na ulimwengu wa nje yalikatizwa na jeshi la lsrael.
Jeshi la Israel limeuvamia kijeshi msafara wa kimataifa wa meli kwa jina la (Sumud) huku utawala huo ukiendeleza mashambulizi na mauaji ya kimbari dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza. Israel imekuwa ikitumia mzingiro dhidi ya Gaza kama njia ya kushadidisha masaibu na mateso kwa wakazi wa eneo hilo.
Wakati huo huo, viongozi wa mataifa mbalimbali wameendelea kulaani hatua hiyo ya Israel.
Colombia imewafukuza wanadiplomasia wa utawala wa kizayuni wa Israel kwa uchokozi uliofanywa na utawala huo ghasibu wa kuuvamia kijeshi msafara wa kimaataifa wa meli unaojulikana kama Sumud uliokuwa ukielekea Ukanda wa Ghaza kwa ajili ya kufikisha misaada ya kibinadamu; sambamba na hilo, serikali ya Bogota imehimiza rais wa Marekani Donald Trump afungwe jela kwa ushiriki wa Washington katika mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na jeshi la kizayuni katika eneo hilo la ardhi ya Palestina.