
Balozi huyo amesema hali iliyoko kwa sasa inaweza kuleta changamoto kubwa kwa Iran, akisema vikwazo vinafungua milango kwa wale wanaotaka kuumaliza mpango wa nyuklia wa Iran, akizungumzia operesheni ya kijeshi ya Israel na Marekani dhidi ya Iran.
Umoja wa Mataifa ulivirejesha vikwazo vyake kwa Jamhuri hiyo ya kiislamu kufuatia mpango wake wa nyuklia.
Mataifa matatu ya Magharibi, Ufaransa, Ujerumani na Uingereza ilivirejesha vikwazo hivyo zikisema Iran imekiuka makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 ambako nchi hiyo ilipaswa kuachana na mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia.
Hata hivyo Iran imekanusha madai ya kutaka kutengezea silaha hizo na kusema hatua ya Magharibi itajibiwa vikali.