Wakati Dkt. Samia Suluhu Hassan, mgombea urais kupitia CCM, anatarajiwa kuanza kampeni zake kesho mkoani Manyara, wananchi wa mkoa huo wameeleza matumaini ya kupatiwa suluhu ya kero mbalimbali zinazowakabili.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Manyara, Peter Toima, amesema wananchi kutoka wilaya zote tayari wameanza kuwasili Babati, makao makuu ya mkoa huo, kwa ajili ya kumpokea mgombea huyo.

Dkt. Samia anatarajiwa kufanya mikutano ya kampeni katika wilaya za Babati na Hanang.

✍ Hellen Kawiche
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *