Mgombea urais kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema serikali yake itaendeleza utalii Arusha kwa kuboresha miundombinu na kuongeza vivutio vipya, ikiwemo utalii wa michezo.
Amesema ujenzi wa uwanja wa michezo wa AFCON umefikia asilimia 63 na utakamilika Julai mwakani, sambamba na ujenzi wa Mji wa AFCON Bondeni City, hatua itakayovutia watalii na wageni zaidi.
Aidha, ameeleza kuwa kuanzia Januari 2026 uwanja wa ndege wa Arusha utaanza kufanya kazi masaa 24, jambo litakaloongeza biashara na usafiri wa watalii.
✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates