
Meneja wa timu ya Taifa ya England, Thomas Tuchel hajamuisha nyota wa Real Madrid, Jude Bellingham katika kikosi chake kinachojiandaa na michezo miwili ya kimataifa mwezi huu.
Katika kikosi cha nyota 24 ambao Tuchel amewaita, jina la Bellingham halipo huku Tuchel akisema hajamuisha kwa sababu za kiufundi.
“Ninafahamu fikra zenu zipo kwa Jude (Bellingham). Ni mchezaji wa kipekee na kwa wachezaji wa kipekee kuna kanuni za kipekee. Lakini kwa kambi hii tumeamua kusimama na uamuzi wetu wa kuikaribisha timu ileile kama ilivyo kw Jude. Mara zote anastahili kuwepo kambini
“Kuna mazingira bado hajapata ubora wake kamili kwa Real Madrid. Hajawahi kumaliza mechi nzima hadi sasa na ameanzishwa katika mechi moja tu hivi sasa.
“Anarudi katika uimara kamili. Tulizungumza kwa simu. Hakuna ishu nje ya hiyo. Amekosa ubora wake,” amesema Tuchel.
Bukayo Saka wa Arsenal amerejea kikosini baada ya kukosekana kilivyoitwa awamu iliyopita kutokana na majeraha.
Hakujawa na nafasi kwa Adam Wharton ambaye ameonyesha kiwango bora akiwa na Crystal Palace lakini pia nyota wa Everton, Jack Grealish hajaitwa.
Licha ya kutokuwa kwenye fomu yake hivi sasa, nyota wa Aston Villa, Morgan Rodgers amejumuishwa katika kikosi hicho cha England.
Oktoba 9 mwaka huu, England itacheza mechi ya kimataifa ya kirafiki na Wales na siku tano baadaye itacheza na Latvia katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia.
KIKOSI KAMILI
Makipa
- Dean Henderson (Crystal Palace)
- Jordan Pickford (Everton)
- James Trafford (Manchester City)
Mabeki
- Dan Burn (Newcastle United)
- Marc Guehi (Crystal Palace)
- Reece James (Chelsea)
- Ezri Konsa (Aston Villa)
- Myles Lewis-Skelly (Arsenal)
- Jarell Quansah (Bayer Leverkusen)
- Djed Spence (Tottenham Hotspur)
- John Stones (Manchester City)
Viungo
- Elliot Anderson (Nottingham Forest)
- Morgan Gibbs-White (Nottingham Forest)
- Jordan Henderson (Brentford)
- Ruben Loftus-Cheek (AC Milan)
- Declan Rice (Arsenal)
- Morgan Rogers (Aston Villa)
Washambuliaji
- Jarrod Bowen (West Ham United)
- Eberechi Eze (Arsenal)
- Anthony Gordon (Newcastle United)
- Harry Kane (Bayern Munich)
- Marcus Rashford (Barcelona)
- Bukayo Saka (Arsenal)
- Ollie Watkins (Aston Villa)