Umoja wa Mataifa umetoa takwimu hizo Alhamisi na kuongeza kuwa raia hao waliuawa baada ya mfululizo wa mashambulizi kupamba moto kati ya jeshi na wanamgambo wanaopigania kuutwaa mji huo.

Kamishna wa Haki za binadamu wa UN ataka hatua za haraka zichukuliwe

Kuhusu ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa Jumamosi, msemaji wa Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk, Seif Magongo alisema,  “Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk, anatoa wito wa kuchukua hatua za haraka ili kuzuia mashambulizi makubwa zaidi ya kikabila na kikatili huko El Fasher, wakati wanamgambo wa RSF wakifanya juhudi za kuchukua udhibiti wa jimbo la Darfur Kaskazini”

Hali ya kiutu mjini El-Fasher ni mbaya, huku mashirika ya kimataifa yakihimiza hatua za haraka za kuwalinda raia na kusitisha mapigano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *