Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa daraja la Msangano lenye thamani ya shilingi bilioni tatu katika barabara ya Chindi–Msangano, Wilaya ya Momba, Songwe.

Daraja hilo litaunganisha Halmashauri ya Tunduma na Makao Makuu ya Wilaya ya Momba, pamoja na tarafa za Msangano na Kamsamba maarufu kwa kilimo cha mazao ya biashara.

Mradi unaotekelezwa na TARURA kupitia tozo ya mafuta ulianza Septemba 2023 na unatarajiwa kukamilika Desemba 2025. Hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 80 na zaidi ya shilingi bilioni 1.5 zimetumika.

✍ Joyce Lyanda
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *