Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Zainab Khamis Shomari, amesema kuwa uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu utakuwa mwepesi kwa chama hicho kutokana na maendeleo makubwa yaliyoletwa na Serikali.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM katika Jimbo la Mtambwe, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba Zainab amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuendelea kukiamini chama hicho, akieleza kuwa maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali yamekuwa yakithibitisha uongozi bora wa CCM kwa wananchi.

Aidha, amewahimiza wananchi wa Jimbo la Mtambwe kuchagua viongozi wa CCM kwenye nafasi zote.

#A#azamtvupdate
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *