Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuendeleza sekta ya utalii mkoani Arusha kwa kukarabati na kupanua viwanja vya ndege vya Lake Manyara wilayani Karatu na Waso, Ngorongoro.

Akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika Karatu, Dkt. Samia amesema zaidi ya shilingi bilioni 88.5 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kurukia ndege, jengo la abiria litakalohudumia watu 150 kwa wakati mmoja, pamoja na barabara ya lami kuelekea uwanja huo ili kurahisisha usafiri wa watalii.

✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *