
Katika video ya moja kwa moja iliyotumwa siku ya Ijumaa, Andry Rajoelina alidai vijana waandamanaji ‘wametumiwa kuchochea mapinduzi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Rais wa Madagascar Andry Rajoelina hii leo Ijumaa ameshutumu, kile alichosema ni jaribio la kupindua serikali yake kufuatia siku kadhaa za maandamano mabaya yanayoongozwa na vijana dhidi ya wasomi wa kisiasa na miaka mingi ya utawala mbaya.
Mikutano ya karibu kila siku ilianza Septemba 25 katika mji mkuu, Antananarivo, kuhusu uhaba wa umeme na maji na tangu wakati huo kuenea katika maeneo mengine ya kisiwa cha Bahari ya Hindi.
Waandamanaji wamemtaka rais ajiuzulu. Yakiitwa kuchukua hatua kwenye mitandao ya kijamii kupitia vuguvugu linaloitwa “Gen Z”, maandamano hayo yalimlazimu Rajoelina kuifuta serikali yake na kukaribisha mazungumzo kurejesha utulivu.
Wametumiwa kuchochea mapinduzi, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 51 alisema akimaanisha waandamanaji ambao wengi wao ni vijana ambao wamejitokeza mitaani kuonyesha hasira zao. “Ninachotaka kukuambia ni kwamba baadhi ya watu wanataka kuharibu nchi yetu,” alisema katika video ya moja kwa moja kwenye ukurasa wake wa Facebook, bila kutaja nani alikuwa nyuma ya hatua hiyo.