Mamilioni ya watu nchini Somalia wanakabiliwa na baa la njaa wakati huu mashirika ya Kimataifa yakipunguza fedha za msaada kuyasaidia mashirika kama WFP kuendelea kutoa msaada.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Shirika la Mpango wa chakula duniani WFP linasema kuanzia mwezi Novemba, watu zaidi ya 750,000 hawatopokea msaada wa vyakula kwa sababu ya ukosefu wa ufadhili kutoka kwa serikali ya Marekani na mataifa mengine ya Magharibi.
WFP inaonya kuwa, hali hii itawaathiri watu ambao tayari wanoishi kwenye mazingira magumu kama wakimbizi, waliokimbia makaazi yao kwa sababu ya njaa, lakini pia changamoto za kiusalama.

Mkurugenzi wa WFP, anayeshughulikia masuala ya dharura, amesema, kiwango cha baa la njaa, kinaongezeka kila siku, na msaada wa shirika hilo, pia unaendelea kupungua kila wakati.
Kwa mujibu wa takwimu za serikali ya Somalia, mpaka mwezi Agosti mwaka huu, watu Milioni 4.4 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.
Kati ya hao, ni watoto Milioni 1.7 chini ya umri wa miaka mitano ambao wanakabiliwa na utapia mlo, wengine wengine zaidi ya Laki nne, ambao hali zao ni mbya.