Kupitia hotuba hiyo aliyoitoa katika ukurasa wake wa Facebook, ameeleza kuwa hakuna anayenufaika kwa kile alichokiita “uharibifu kwa taifa.” Kiongozi huyo amesema maandamano hayawezi kutatua changamoto za nchi hiyo bali mazungumzo.

Awashutumu wapinzani kwa jaribio la mapinduzi

Bila ya kutoa ushahidi Rais Rajoelina hivi karibuni aliwashutumu baadhi ya wanasiasa nchini humo kwa hujuma za kutaka kutumia maandamano hayo kufanya mapinduzi.

Maandamano yaliyoanza Madagascar wiki iliyopita yameendelea kusambaa ambapo raia wanapinga umasikini na rushwa. Rais Rajoelina hata hivyo ameipuuza miito ya waandamanaji ya kumtaka aondoke madarakani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *