
WFP limesema idadi ya watu wanaopokea msaada wa dharura wa chakula itapunguzwa kutoka milioni 1.1 hadi watu 350,000 katika mwezi wa Novemba kutokana na ukosefu mkubwa wa fedha za ufadhili. Mamilioni ya watu wanakabiliwa na athari mbaya zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi na baa la njaa nchini Somalia.