Katika hotuba yake Merz amesisitiza pia umuhimu wa Ujerumani kuzingatia demokrasia na utawala wa sheria. Matamshi hayo ameyatoa wakati wa maadhimisho ya miaka 35 tangu zilizokuwa Ujerumani Mashariki na Magharibizilipoungana na kuwa taifa moja.

Merz ahimiza demokrasia na utawala wa sheria

Amenukuliwa akisema, “Tunataka kuwa taifa la Ulaya ambalo liko wazi kwa ulimwengu. Kwa sababu ya hilo, demokrasia, utawala wa sheria, uvumbuzi na mshikamano ndiyo masuala yanayolikamilisha bara la Ulaya. Hii ni Ulaya na huu ndiyo mtindo wa maisha wa Ulaya.”

Merz ameyasema hayo katika hafla iliyofanyika mjini Saarbrücken iliyohudhuriwa pia na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. Kansela Merz pia ametoa wito kwa Wajerumani kuwajibika katika kukabiliana na kitisho cha kiusalama kwa kujitolea jeshini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *