Ujumbe wa madaktari bingwa, wataalamu na watoa huduma za afya 52 umeondoka nchini kuelekea visiwa vya Anjouan, Comoro kwa lengo la kutoa matibabu ya magonjwa mbalimbali huku pia wakikuza dhana ya utalii tiba kimataifa.
Ujumbe huo umejumuisha wataalamu kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI), Bohari ya Taifa ya Dawa (MSD), Hospitali ya Benjamin Mkapa, Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, wakiwa tayari kutoa huduma za matibabu ya kisasa kwa wagonjwa wa Comoro.
#AzamTVUpdates
✍Estabela Malisa
Mhariri | John Mbalamwezi