Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Sweden Alexander Isak, mwenye umri wa miaka 25, ameiambia Newcastle kwamba bado anataka kuondoka na kujiunga na Liverpool licha ya jitihada za mwenyekiti wa klabu Yasir Al-Rumayyan na kikao na mmoja wa wamiliki wenza Jamie Reuben. (Telegraph)
Manchester United imefikia makubaliano ya awali na Real Betis kwa ajili ya winga wa Kibrazili Antony, 25, kurejea katika klabu hiyo ya Hispania kwa mkopo wenye sharti la kununuliwa moja kwa moja. (Telegraph)
Manchester United pia inatarajia kukubaliana masharti binafsi na kipa Senne Lammens ili kumsajili mchezaji huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 23 kutoka Royal Antwerp kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Telegraph)
Real Madrid na Atletico Madrid wanamfuatilia kiungo wa timu ya taifa ya Uingereza Kobbie Mainoo, 20, wa Manchester United ambaye anataka kuondoka baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha Old Trafford. (Mail)
Mainoo pia anasakwa Fulham, sambamba na winga wa Kiingereza wa Arsenal Reiss Nelson, 25. (Teamtalk)
Porto wako karibu kufikia makubaliano ya mkopo yenye sharti la kumnunua moja kwa moja beki wa Poland Jakub Kiwior, 25, wa Arsenal. (Sky Sports)
Chanzo cha picha, Getty Images
Crystal Palace wanajiandaa kwa mazungumzo na Liverpool kuhusu kiungo mshambuliaji Mwingereza Harvey Elliott, 22, wakiharakisha mipango ya kumpata mrithi wa Eberechi Eze, 27, ambaye amejiunga na Arsenal. (Football Insider)
Brentford wanamfikiria mshambuliaji wa Ujerumani Max Beier, 22, wa Borussia Dortmund, huku klabu hiyo ya Bundesliga ikiwa karibu pia kukamilisha dili la kumsaini mshambuliaji wa Ureno Fabio Silva, 23, kutoka Wolves. (Sky Sports)
Roma wamefanya mazungumzo na Chelsea pamoja na wawakilishi wa Tyrique George kuhusu kumsaini winga huyo wa Kiingereza mwenye umri wa miaka 19. (Gianluca di Marzio)
Alejandro Garnacho amekataa ofa mpya kutoka klabu moja ya Saudi Pro League katika saa 48 zilizopita huku mazungumzo kati ya Manchester United na Chelsea kuhusu winga huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 21 yakiwa yamefikia hatua za mwisho. (Fabrizio Romano)
Bayer Leverkusen na Galatasaray wako tayari kushindana na Crystal Palace kumsajili beki wa Manchester City na timu ya taifa ya Uswizi Manuel Akanji, 30. (Independent)
Chanzo cha picha, Getty Images
West Ham wako karibu kukamilisha dili la paundi milioni 17.3 kumsajili kiungo wa Kifaransa Soungoutou Magassa, 21, kutoka AS Monaco. (Guardian)
Dili la mkopo kwa kiungo mkabaji wa Ivory Coast Ibrahim Sangare, 27, wa Nottingham Forest pia linafuatiliwa na West Ham, ambao pia wanavutiwa na kiungo wa Mfaransa Junior Mwanga, 22, wa Strasbourg na kiungo Mwingereza Hayden Hackney, 23, wa Middlesbrough. (Sky Sports)
Nottingham Forest wamekataliwa ofa ya awali ya karibu paundi milioni 10 kwa ajili ya beki wa kulia Muitaliano Nicolo Savona, 22, kutoka Juventus. (Gianluca di Marzio)
Crystal Palace wamefikia makubaliano ya awali na Villarreal kwa ajili ya kiungo wa Kihispania Yeremy Pino, 22, kwa dau linaloweza kufikia paundi milioni 26. (AS)
Kiungo wa Liverpool James McConnell, 20, anatarajiwa kujiunga na Ajax kwa mkopo kwa msimu wa 2025-26 baada ya nyota huyo wa kimataifa huyo wa England chini ya miaka 20 kusaini mkataba mpya wa miaka mitano na klabu hiyo. (Athletic)