Wazazi na walezi wa wanafunzi wa kidato cha nne wanaotarajia kuhitimu wametakiwa kutimiza wajibu wao katika malezi, ili vijana hao watumie muda kwa manufaa na kuepuka kujiingiza kwenye vitendo visivyo na maadili.

Imeelezwa kuwa malezi duni yamechangia mmomonyoko wa maadili miongoni mwa vijana kutokana na kukosekana usimamizi wa karibu.

Wito huo umetolewa katika mahafali ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Kizuka iliyoko Morogoro.

✍ Theresia Mwanga
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *