#HABARI: Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Lupa Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya Masache Njelu Kasaka amefanikiwa kurudisha Fomu kwenye Ofisi ya Msimamizi Msaidizi wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Msimamizi Msaidizi wa Tume Huru ya Uchaguzi Jimbo la Lupa Athumani Bamba, amemteua na Kumtangaza Mgombea wa CCM Masache Kasaka kuwa Mgombea pekee wa Ubunge Jimbo la Lupa. Wagombea toka vyama vya CCM na ACT Wazalendo, walichukua Fomu Tarehe 25 Agosti na Mgombea wa CCM Ndg. Kasaka ndiye aliyerudisha Fomu Peke yake leo Tar 27 August, ikiwa ni Siku ya Mwisho ya kurudisha Fomu na Uteuzi.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania