#HABARI: Baadhi ya waendesha ghala kutoka mikoa ya Mwanza na Geita, wameiomba serikali kuongeza juhudi za kutoa elimu kwa wakulima wa zao la dengu juu ya umuhimu na faida ya mfumo wa Stakabadhi Ghalani, wakisisitiza kuwa wakulima wengi bado hawana uelewa wa kutosha kuhusu mfumo huo.
Baadhi ya waendeshaji wa maghala wamesema kuwa ingawa mfumo wa Stakabadhi Ghalani umeonyesha mafanikio katika maeneo mengine ya kilimo, bado wakulima wengi wa dengu wanauacha na kuendelea kuuza mazao yao kwa watu wa kati.
Wameeleza kuwa hali hiyo inawanyima wakulima faida stahiki kwani wanunuzi wa kati huweka bei ya mazao kwa manufaa yao binafsi, hali inayodidimiza kipato cha mkulima.
Wamesema iwapo serikali itapanua elimu ya mfumo huu hadi Vijijini na kwa lugha rahisi kueleweka wakulima wataweza kuelewa thamani ya mazao yao na namna ya kuyauza kwa njia salama na yenye tija zaidi.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania