Chanzo cha picha, Getty Images
-
- Author, Adam Millington
- Nafasi, Mwandishi BBC Sport
Manchester United imepata mshtuko mkubwa baada ya kuondolewa katika kombe la EFL kupitia mikwaju ya matuta na timu ya Grimbsby ambayo ni kiwango cha chini mara 20 ukilinganisha na Man United- matokeo ambayo yatasalia kumbukumbu miaka ijayo katika historia ya soka duniani.
United walipigwa mikawaju 12 dhidi ya 11 katika awamu ya matuta, baada ya kujizatiti kusawazisha mabao mawili na kuwapa sare na Grimsby.
Lakini hili sio mara ya kwanza kwa United kufungwa katika mechi za nyumbani.
Je, unakumbuka ilivyofungwa mabao 3-0 na New York city katika uwanja wa Trafford miaka 30 iliyopita?
Baada ya Grimsby kuishinda United, BBC Sport inaangazia vipigo 10 visivyosahaulika katika kombe la FA na EFL.
Hii sio orodha kamili, unaweza kutoa maoni yako na kuorodhesha vipigo kumi ambavyo wewe hujavisahau hadi sasa.
Grimsby 2-2 Man Utd (12-11 kwa mikwaju ya penalti, Kombe la Ligi, 2025)
Matokeo haya yalishangaza si tu kwa jinsi yalivyotokea bali pia kwa ukubwa wake.
Grimsby Town, timu ya Ligi ya Pili, iliishinda Manchester United kutoka Ligi Kuu.
Sio kwamba walishinda tu, Grimsby walitoka kifua mbele, wakifunga mabao mawili ya haraka kupitia Charles Vernam na Tyrell Warren ndani ya dakika 30 za kwanza.
Bryan Mbeumo akarejesha matumaini kwa United kabla ya Harry Maguire kusawazisha dakika ya 89.
Penalti zikafuata, ikageuka pambano la kusisimua, kila mchezaji wa pande zote akapiga. Oduor (Grimsby) na Cunha (Man Utd) ndio pekee walikosa kati ya wachezaji 11 wa kila upande waliopiga.
Wachezaji walirudia tena penalti na baada ya Darragh Burns kufunga penalti ya 12-11, Mbeumo aligonga mwamba na Grimsby wakashinda.
Plymouth 1-0 Liverpool (Kombe la FA, 2025)
Kocha wa Liverpool Arne Slot alibadilisha wachezaji 10 katika kikosi cha timu yake baada ya ushindi wao katika nusu fainali ya Kombe la EFL, na Liverpool wakalipa gharama.
Dakika nane baada ya mapumziko, Plymouth walipata penalti kufuatia Harvey Elliot kugusa mpira kwa mkono, na Ryan Hardie aliopewa fursa alifunga penalti hiyo kwa ustadi mkubwa.
Hardie karibu aongeze bao la pili muda mfupi baadaye lakini kipa Caoimhin Kelleher aliokoa kwa kugusa mpira uliogonga mwamba.
Klabu hiyo iliyoko mkiani mwa Ligi kuu ya Uingereza ilishikilia ushindi huo, huku kipa Conor Hazard akifanya uokoaji wa muhimu mwishoni, na kuwatoa Liverpool ambao baadaye walishinda ubingwa wa Ligi Kuu.
Chelsea 2-4 Bradford City (Kombe la FA, 2015)
Bradford walikuwa nafasi ya 49 nyuma ya Chelsea waliposafiri hadi Stamford Bridge kukutana na Chelsea viongozi wa Ligi Kuu wakati huo.
Gary Cahill na Ramires waliifungia Chelsea na kuwapa uongozi wa mabao 2-0 katika mechi ya mzunguko wa nne.
Lakini Bradford walikuwa na mipango mingine.
Jon Stead alifunga bao la kwanza, Filipe Morais akasawazisha, Andy Halliday akaongeza la tatu, na Mark Yeats akahitimisha kwa bao la nne, na kuwapa ushindi mkubwa dhidi ya kikosi cha Jose Mourinho.
Oldham 3-2 Liverpool (Kombe la FA, 2013)
Liverpool, klabu kubwa ya Ligi Kuu, walikuwa na nyota kama Luis Suarez, Raheem Sterling na Daniel Sturridge wakianza mchezo.
Oldham, kutoka Ligi ya Kwanza, walikuwa wakikabiliwa na matatizo ya kifedha lakini walicheza kwa ari ya hali ya juu.
Matt Smith alifunga kwa kichwa baada ya kupatiwa mpira na Youssouf M’Changama.
Suarez alisawazisha, lakini Smith alifunga tena baada ya makosa ya mlinda lango Brad Jones.
Reece Wabara aliongeza bao la tatu kwa Oldham na kuioa ushindi wa mapema Latics mabao matatu dhidi ya moja kabla ya Joe Allen kuvutia moja nyuma kwa Liverpool.
Hata hivyo, hata kumuingiza Steven Gerrard hakukuwa msaada wa kutosha kwa Liverpool kuepuka kipigo.
Bradford City 1-1 Arsenal (3-2 kwa penalti, Kombe la Ligi, 2012)
Timu ya daraja la nne dhidi ya Arsenal ya Ligi Kuu katika robo fainali, Arsenal walikuwa wanaonekana kuwa watashinda mechi hiyo.
Lakini Bradford tayari walikuwa wamesababisha mshangao kwa kuwatoa Wigan kwa penalti katika raundi ya awali.
Walikuwa tayari kumenyana na vijana wa Arsene Wenger.
Garry Thompson aliwapa Bradford uongozi, lakini Thomas Vermaelen alisawazisha kwa kichwa dakika mbili kabla ya mwisho wa muda wa kawaida.
Kama Mbeumo wa United alivyokosa penalti muhimu dhidi ya Grimsby baada ya kufunga katika muda wa kawaida, ndivyo ilivyotokea kwa Vermaelen pia.
Bradford wakashinda 3-2 kwa penalti.
Baadaye waliwatoa Aston Villa katika nusu fainali kabla ya kufungwa 5-0 na Swansea kwenye fainali ya Wembley.
Liverpool 2-2 Northampton ( 2-4 kwa penalti, Kombe la Ligi, 2010)
Hii ilitokea pale pale Anfield.
Liverpool wakafunga mapema kupitia Jovanovic, lakini Billy McKay akasawazisha.
Northampton wakaenda mbele kupitia Michael Jacobs, Ngog akasawazisha dakika za mwisho.
Penalti zikaja na Northampton wakaibuka kidedea.
Abdul Osman akafunga penalti ya ushindi.
Man Utd 0-3 York City (Kombe la ligi, 1995)
Ruben Amorim sio kocha wa kwanza Man United kupata kipigo cha aibu.
Hata Sir Alex Ferguson aliwahi kushtuliwa!
York City waliwavaa United wakiwa na kikosi cha mastaa kama David Beckham, Ryan Giggs na Lee Sharpe.
Paul Barnes, babake mzazi wa winga wa Newcastle Harvey Barnes akafunga mabao mawili, moja kwa penalti, Tony Barras akaongeza la tatu na kuipiga katika uwanja wa Old Trafford.
Katika marudiano, United walileta timu iliyo na ujuzi zaidi akina Eric Cantona, Paul Scholes akafunga mabao mawili, lakini York wakaenda mbele kwa jumla ya 4-3, wakifunga bao muhimu kupitia Scott Jordan.
Wrexham 2-1 Arsenal (Kombe la FA, 1992)
Arsenal walikuwa mabingwa wa Ligi Kuu, Wrexham wa mwisho kabisa Daraja la Tatu.
Wanabunduki walisafiri hadi Wales wakiwa na nafasi nzuri ya ushindi.
Alan Smith akafunga kwa Arsenal, lakini dakika 10 kabla ya mwisho, Mickey Thomas akapiga mkwaju wa yadi 25 ukamshinda David Seaman.
Dakika mbili baadaye, Steve Watkin akaandika historia kwa bao la ushindi.
Sutton 2-1 Coventry (Kombe la FA, 1989)
Sutton nao walikuwa katika hali nzuri katika mashindano ya kombe la 2016-17, hawatawahi kusahau baada ya kufunga timu tatu za EFL ikiwemo Leeds United kabla ya kushindwa na Arsenal raundi ya tano.
Pia walifanya makeke yao na kuandika historia katika ulingo wa soka.
Sutton United, timu ya daraja la chini kabisa, waliwatoa Coventry waliokuwa wanacheza Ligi Kuu na mabingwa wa FA mwaka 1987.
Matthew Hanlan akaweka bao la ushindi kwa mkwaju mzuri, na Sutton wakatengeneza hadithi ya kusimulia miaka mingi.
Hereford 2-1 Newcastle (Kombe la FA, 1972)
Newcastle walikuwa wa Ligi Kuu, na walifungwa katika raundi ya tatu ya kombe la FA baada ya kuishambulia Hereford United mwaka 1972.
Mechi ya kwanza kati ya Hereford na New castle ilimalizika kwa sare ya mabao mawili katika uwanja wa St James, na kwenye marudiano, McDonald akaipa Newcastle uongozi.
Lakini Ronnie Radford akapiga mkwaju maarufu la yadi 30 na kusawazisha, kabla ya Ricky George kufunga la ushindi katika muda wa nyongeza.
Shangwe zikatawala Edgar Street.
Hereford ikawa klabu ya kwanza isiyo ya ligi kushinda timu ya Daraja la Kwanza tangu 1949.
Imetafsiriwa na Mariam Mjahid