Kama unataka kutazama mbashara Fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico mwakani unapaswa kuandaa fungu la kutosha ili uweze kumudu gharama za usafiri, malazi na tiketi katika muda utakaokuwepo huko.

Ukiweka kando gharama za huduma za malazi na usafiri ambazo zinatofautiana kutegemea na Shirika la Ndege ambalo shabiki atatumia kutoka nchini mwake kwenda katika nchi hizo au hoteli atakayofikia akiwa huko, gharama za tiketi za kutazama mechi nazo zimechangamka.

Imefichuka kwamba tiketi ya bei ya chini ya kutazama mechi za mashindano hayo itauzwa kiasi cha Dola 60 (Sh147,300).

Bei hiyo ni kwa jukwaa la daraja la nne na ni kwa mechi za hatua ya makundi tu na kwa daraja hilo, gharama ya juu ya tiketi ni Dola 140 (Sh343,700).

Bei ya tiketi katika hatua ya makundi kwa jukwaa la daraja la tatu inaanzia Dola 120 (Sh294,600) hadi Dola 280 (Sh687,400).

Katika hatua ya makundi, tiketi ya Jukwaa la Daraja la Pili itauzwa kati ya Dola 260 (Sh638,300) hadi Dola 605 (Sh1.5 milioni) na tiketi ya Jukwaa la Daraja la Kwanza itauzwa kati ya Dola 345 (Sh846,975) hadi Dola 805 (Sh2 milioni).

Gharama ya chini ya tiketi katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo ambao utaihusisha timu ya Taifa ya Mexico kwa Jukwaa la Daraja la Nne itauzwa kwa Dola 370 (Sh908,350).

Kwa mechi ya ufunguzi ambayo itafanyika Canada ikihusisha timu ya Taifa ya nchi hiyo, gharama ya chini ya tiketi kwa Jukwaa la Daraja la Nne itauzwa kwa kiasi cha Dola 355 (Sh871,525).

Mchezo wa ufunguzi ambao utaihusisha timu ya taifa ya Marekani, tiketi ya bei ya chini zaidi ni Dola 560 (Sh1.4 milioni).

Tiketi ya bei ya juu zaidi katika Fainali za Kombe la Dunia ni ya Jukwaa la Daraja la Kwanza katika mechi ya fainali ambayo itauzwa kiasi cha Dola 6,370 (Sh16 milioni).

Mchanganuo wa gharama za tiketi kombe la dunia 2026

                       Daraja 1     Daraja 2      Daraja 3     Daraja 4

Ufunguzi Mexico       Sh4.5 mil     Sh3 mil       Sh1.8 mil    Sh907,710

Ufunguzi Canada        Sh4 mil      Sh3 mil       Sh1.8 mil    Sh870,911

Ufunguzi Marekani     Sh7 mil       Sh4.8 mil     Sh2.7 mil    Sh1.2 mil

Hatua ya Makundi     Sh846,378     Sh637,850      Sh294,392    Sh147,182

Mshindi wa Tatu      Sh2.5 mil     Sh1.8 mil      Sh883,177    Sh404,789

Fainali              Sh16 mil      Sh10 mil       Sh6.9 mil    Sh4.5 mil

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *