Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea wamekubali mkataba wa kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wa Senegal Nicolas Jackson, 24, kwenda Bayern Munich . (Bild – in Germany)
Kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 20, atafikiria kuondoka Manchester United katika wiki ya mwisho ya dirisha la uhamisho ikiwa klabu hiyo itapokea ofa inayofaa. (,Sport)
Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambulizi wa Manchester United na Denmark Rasmus Hojlund, 22, atapata nyongeza ya mshahara iwapo atakubali kujiunga na Napoli kabla ya tarehe ya mwisho ya kuhama. (Gazzetta dello Sport – in Italian)
Crystal Palace watoa ofa ya pauni milioni 15 kwa mlinzi wa Uswisi wa Manchester City Manuel Akanji, 30. (Sun )
Chanzo cha picha, Getty Images
Strand Larsen ana nia ya kuhamia Newcastle huku Magpies wakiweka dau jingine, lakini hatazamiwi kuwa kama kiungo mbadala wa moja kwa moja wa mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 25, ambaye anasakwa na Liverpool. (subsription required)
Millwall inatazamiwa kumsajili kipa Joel Coleman mwenye umri wa miaka 29, ambaye amekuwa hana klabu tangu aondoke Bolton . ( Pete O’Rourke)
Watford wanatazamiwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Georgia chini ya umri wa miaka 19, Nikoloz Chikovani kutoka Dinamo Tbilisi, 18 na kumpeleka nje kwa mkopo. ( (Watford Observer )
Chanzo cha picha, Getty Images
Tottenham inaweza kukabiliwa na kukataliwa kutoka kwa walengwa wa nne kuu baada ya Como kukataa ofa ya pauni milioni 50 kutoka kwa Spurs kwa kiungo wa kati wa Argentina Nico Paz, 20. (Mirror)
Wolves itampa mshambuliaji Jorgen Strand Larsen kandarasi mpya baada ya kukataa ofa ya pauni milioni 50 kutoka kwa Newcastle lakini bado wanaweza kushawishika kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway, 25 iwapo watapata ofa ya zaidi ya pauni milioni 75. (Telegraph – subsription required)
Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Brazil Andreas Pereira, 29, ataruhusiwa kuondoka Fulham msimu huu wa kiangazi. (Team Talk)
Maafisa wa Newcastle , akiwemo mmiliki mwenza Jamie Reuben, wamezungumza na Isak nyumbani kwa mshambuliaji huyo ili kumshawishi kusalia katika klabu hiyo na kurejea kwenye kikosi cha Eddie Howe licha ya Liverpool kumtaka. (Daily Mail
Chanzo cha picha, Getty Images
Borussia Dortmund wanakaribia kufikia makubaliano na Wolves kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Ureno Fabio Silva, 23. ( Athletic – subcription required)
Beki wa Everton na Scotland Nathan Patterson anasakwa na Sevilla ambao wanatafuta mkataba wa mkopo kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Liverpool Echo)
West Ham wamekataa ombi la Everton la kumnunua kiungo wa kati wa Czech Tomas Soucek, 30. (Time – subcription required )
Chanzo cha picha, Getty Images
Wakurugenzi wa Roma watafanya mkutano na Liverpool kuhusu mpango wa kumnunua beki wa kushoto wa Ugiriki Kostas Tsimikas huku Marseille pia ikimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (Football Italia)
Crystal Palace wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kumsajili beki wa kati wa Toulouse Mfaransa Jaydee Canvot, 19, baada ya ofa ya Aston Villa kukataliwa. (Fabrizio Romano)
Kiungo wa kati wa Bournemouth Philip Billing, 29, anatazamiwa kurejea nchini kwao Denmark na kujiunga na Midtjylland kwa mkataba wa £5m. (Time- subcription required )
Chanzo cha picha, Getty Images
Derby County wamekubali mkataba wa £3.5m na klabu ya Austria Sturm Graz kumnunua beki wa kulia wa Scotland Max Johnston, 21, ambaye anatazamiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kabla ya kusaini mkataba wa miaka minne. (Sky Sports )
Sheffield United imewachukua wachezaji wa zamani wa kimataifa wa Uingereza Danny Ings na Nathan Redmond kwa majaribio, wawili hao walishawahi kufanya kazi na Ruben Selles huko Southampton. ( Sheffield Star)