#HABARI: Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Kamishna msaidizi Mwandanizi wa Polisi (SACP) Marco G. Chilya, amewataka watendajiwa wa Dawati la Jinsia na watoto Mkoani Ruvuma kuendelea kujikita katika utoaji elimu juu ya madhara ya ukatili wa Kijinsia, unyanyasaji katika Jamii na kujenga mahusiano mazuri kwa jamii zinayowazunguka ili kuweza kupata taarifa za uhalifu na wahalifu ili ziweze kuzuiliwa kabla ya kuleta madhara makubwa kwa wahanga.
Kamanda Chilya (SACP) amewataka kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia haki, weledi na uadilifu kwa wale wote wanaowahudumia kwa kutoa huduma bora kwa waathirika wa ukatili pamoja na kutunza siri za wale wote wanaotoa taarifa za ukatili ikiwa ni pamoja na wale wanaowahudumia.
Kwa upande wake Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Ruvuma Mrakibu msaidizi wa Polisi (ASP) Odilia Mroso, amesema atahakikisha anaendelea kusimamia mipango kazi ya utoaji elimu ya ukatili na madhara yake kwa watendaji wa kila Wilaya ili kuweza kuepukana na vitendo vya uhalifu vitokanavyo na Ukatili baina ya Wananchi.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania