Chanzo cha picha, Getty Images
Mnamo Desemba 14, 1929, gazeti la Marekani la ‘The New York Times’ lilichapisha habari ambazo ziliishtua Marekani pamoja na watu wa Hungary, nchi iliyopo umbali wa maelfu ya kilomita.
Kulingana na habari, kesi imefunguliwa dhidi ya wanawake wapatao 50.
Wanawake hao wote wanatuhumiwa kwa kuwatia sumu na kuwaua wanaume wengi waliokuwa wakiishi katika kijiji kimoja huko Hungary, Ulaya.
Bila shaka, habari hii ilikuwa fupi, lakini ilikuwa na habari nyingi.
Ripoti hiyo ilisema kuwa kati ya 1911 na 1929, wanawake kadhaa waliwapa sumu zaidi ya wanaume 50 katika kijiji kiitwacho Nagyrev, karibu kilomita 130 kusini mwa Budapest, mji mkuu wa Hungary.
Wanawake hawa wanajulikana kama ‘watengenezaji wa malaika’. Waliua wanaume baada ya kuchanganya suluhisho la arseniki na sumu.
Chanzo cha picha, Getty Images
Uchunguzi ulianza baada ya miaka mingi
Baadhi ya watu wameelezea tukio hili kuwa mauaji makubwa zaidi ya wanaume katika historia ya hivi karibuni.
Baada ya kesi kufunguliwa dhidi ya kundi la wanawake, jina moja liliendelea kuja. Lilikuwa jina la Jojasana Fajakas mkunga kutoka kijijini.
Wakati huo, kijiji hiki kilikuwa sehemu ya Dola ya Austro-Hungarian. Hakukuwa na daktari wa ndani. Wakunga walikuwa wakisimamia afya ya eneo hilo na kuwatibu watu.
Akizungumza na kipindi cha redio cha BBC, Mnamo mwaka wa 2004 , mkazi wa kijiji Maria Gunya, alisema kuwa Fajakas ndiye mhusika mkuu wa kulaumiwa kwa sumu hiyo, kwa ababu wanawake wa kijiji hicho wangezungumza waziwazi na Fajakas matatizo yao ya kibinafsi na yale ya waume zao.
Gunaya alisema Fajakas aliwaeleza wanawake kwamba ikiwa walikuwa na matatizo na waume zao, kuna suluhu rahisi.
Ingawa Fajakas alisemekana kuwa mshukiwa mkuu wa mauaji haya ya halaiki, ushuhuda wa wanawake wa kijiji katika nyaraka za kesi ulifichua visa vingi vya kutisha vya unyanyasaji, mateso, ubakaji na unyanyasaji wa wanaume dhidi ya wanawake wa kijiji hicho.
Iliripotiwa kuwa wanawake walikabiliwa na dhuluma kali nyumbani, ikiwa ni pamoja na kupigwa na kubakwa.
Kulingana na Gunaya, tatizo kubwa lilikuwa kwamba ndoa wakati huo mara nyingi zilipangwa kwa matakwa ya familia na si kwa uchaguzi wa pande zote mbili. Wasichana wengi wachanga waliolewa na wanaume wenye umri mkubwa zaidi yao.
Gunaya alisema kwamba talaka haikuwezekana wakati huo. Haijalishi ni kiasi gani wanawake walinyanyaswa, bila kujali jinsi walivyodhalilishwa, hakukuwa na tumaini la talaka.
Lakini ripoti zilizoandikwa wakati huo zilifichua kwamba kasoro fulani ilikuwa kwamba wakati huo, ndoa mara nyingi zilitegemea aina fulani ya mkataba, kama vile ardhi, urithi, na wajibu mwingine wa kisheria.
Hata hivyo, jambo hili halikuonekana kwa miaka mingi. Kulingana na ripoti za polisi, mauaji ya kwanza yalitokea mwaka wa 1911. Hata hivyo, uchunguzi haukuanza hadi 1929.
Gunya aliiambia BBC kuwa Fajakas alianza kuwapa wanawake imani kwamba wanaweza kutatua matatizo yao.
Kesi ya kwanza ya mtu aliyetiwa sumu katika kijiji cha Fajkas ilitokea mwaka wa 1911. Baada ya hapo, wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia na kuanguka kwa Milki ya Austro-Hungary, matukio hayo yaliongezeka. Mauaji ya wanaume yaliongezeka.
Kwa njia mtindo huu , wanaume 45 hadi 50 walikufa katika miaka 18. Wanaume waliokufa walikuwa mababa. Wote walizikwa kwenye makaburi ya kijiji. Watu wengi walianza kuita kijiji cha Nagyarevo ‘mji wa wauaji’.
Polisi waligundua matukio haya na kujaribu kumkamata mwanamke huyo, lakini alipogundua kuwa alikuwa akisakwa, alikunywa sumu na kujiua.
Katika miaka ya 1950, mwanahistoria Ferenc Gerogev alikutana na mzee kutoka kijijini hicho alipokuwa gerezani chini ya utawala wa kikomunisti.
Mkulima huyo mzee alidai kuwa wanawake wa Nagyarevo wamekuwa wakiwaua waume zao tangu zamani.
Baadhi ya miili pia ilitolewa kwenye makaburi katika mji wa karibu wa Tiszakurt, ambapo sumu pia ilipatikana. Lakini hakuna aliyeadhibiwa kwa mauaji yao.
Kulingana na baadhi ya makadirio, jumla ya vifo vinavyotokana na sumu katika eneo hilo vimefikia 300.