Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Filippo Grandi, amewasili Goma, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), siku ya Ijumaa, Agosti 29. Amewatembelea watu waliokimbia makazi yao waliokuwa wamerejea Saké, takriban kilomita 20 kutoka Goma, na kusikitishwa na hali yao ya maisha, huku wengi wao wakiishi kwenye vibanda vya maturubai bila msaada wowote.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Filippo Grandi ametoa wito kwa mashirika yanayojihusisa na misaada ya kibinadamu kuungana kusaidia watu hawa, ambao wanatatizika kupata mahitaji ya kimsingi kama vile chakula na kulala. Kwa wengi wao, nyumba zao ziliharibiwa wakati wa mapigano ya hivi majuzi kati ya waasi wa AFC/M23 na jeshi la Kongo.

Baada ya kuzuru mji wa Sake, mwakilishi wa UNHCR amezungumza na mamlaka ya kundi la AFC-M23.

Huu ni wito kwa wafadhili kuyapa mashirika ya kibinadamu uwezo muhimu ili kuwasaidia watu hawa. Pia ni wito kwa pande zote zinazohusika katika mazungumzo ya amani ya Washington na Doha kuhakikisha kwamba, katika mijadala yote hii, ambayo kwa hakika inahusu nyanja za kisiasa, kiuchumi na kiusalama, zisisahau hali ya watu wanaoteseka, wanaohitaji msaada wa haraka wa kibinadamu, na ambao—hasa wakimbizi wa ndani na watu waliokimbia makazi yao—wanahitaji ufumbuzi wa haraka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *