Katikati ya mwezi wa Agosti, serikali ya Mali ilitangaza kuwa imezuia “jaribio la kuhatarisha usalama wa taasisi za Jamhuri.” Wanajeshi kadhaa wakiwemo majenerali wawili walikamatwa. Miongoni mwa wale wanaoshutumiwa kushiriki katika “jaribio” hili ni raia wa Ufaransa aliyewasilishwa kama mmoja wa wachochezi wa operesheni hiyo. Paris inakanusha hili na inaelezea wasiwasi wake juu ya hatima ya mwanadiplomasia wake.
